Baada ya Mashabiki na wanachama mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Simba Sports Club kuchoshwa na kile kinachoitwa kufanya vibaya kwa timu yao katika mechi za ligi kuu Tanzania Bara (VPL), mashabiki hao wameamua kutumia haki yao ya kikatiba ya kuutaka uongozi wa klabu hiyo kuitisha mkutano mkuu ili kujadili mustakabali wa klabu hiyo katika mbioa za kuwania ubingwa wa ligi kuu.
Nia hiyo ya wanachama hao kutaka uongozi kuitisha mkutano huo inakuja wakati ambao Mabingwa wameambulia matokeo mabaya dhidi ya Toto Afrika ya Mwanza pamoja na kutoshana nguvu na Wana-lamba lamba wa Chamazi, Azam FC huku baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wakishutumiwa kuhusika kuihujiumi timu hiyo.
|
No comments:
Post a Comment