Monday, November 12, 2012

VYAKULA BEI JUU DAR, WIZARA YAKIRI KUNA TATIZO


Afisa Habari wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bw. Richard Kusaga (Pichani: Juu) amesema Wizara hiyo imejipanga kupunguza ongezeko la bei ya vyakula nchini kote licha ya gharama za za usafirishaji wa mazao ya vyakula na bei ya mafuta kupanda nchini.

Kauli ya Afisa Habari wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika imekuja pindi ambapo gharama za vyakula zinazidi kupanda kila kukicha hivyo kuwafanya wananchi wengi wenye kipato cha chini kushindwa kumudu gharama za maisha na na mahitaji ya familia huku wengi wao wakiinyoshea vidole Serkali kwa kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei unaotajwa kuwa chanzo cha tatizo hilo.

Bw. Richard Kusaga amesema hayo wakati akijibu maswali ya  Waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Makao Makuu ya Wizara hiyo waliotaka kujua ni hatua zipi Wizara hiyo inazifanya ili bei ya Vyakula isizidi kupanda kila kukicha nchini kote.

Baada ya kufanya mahojianoo na Afisa Habari wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Mwanablogu alipata wasaha  kuzungukia maeneo ya Sokoni, na hizii ndizo zilikuwa bei za vyakula kwa siku ya leo katika soko la Magomeni Mikumi jijini Dar-es-salaam.

1. MCHELE WA MBEYA (SUPER)-1700@Kilo 1
2. MCHELE WA MBEYA (KYELA)-1800@Kilo 1
3. MAHARAGWE (SOYA)-1700@Kila 1
4. NJEGELE-1500@Kilo 1
bei haikamatiki!!!!!!


No comments:

Post a Comment