Tuesday, November 27, 2012

UCHUMI WA TANZANIA WAENDELEA KUIMARIKA


Utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia unaonesha kuwa uchumi wa Tanzania unaendelea kukua kwa kiwango cha silimia 6 kwa kipindi cha mwaka uliopita licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali za kiuchumi.  

Taarifa ya Benki ya Dunia inaeleza kwamba kasi hiyo ya ukuaji uchumi inatokana na uwezo wa Serikali kufanya mabadiliko yanayostahili katika kutumia sera za hazina na fedha, hususani katikati ya ongezeko kubwa la mfumuko wa bei unaoonekana kuanzia Mwezi Novembe, 2011.

Katika mkutano wake na Wahariri wa vyombo vya habari, Mchumi Mkuu wa wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, Bw. Jacques Morisset, amesema," ukuaji wa uchumi unaofikia asilimia 6.5 kwa kipindi cha mwaka 2011/12, na nakisi ya hazina na fedha za matumizi ya kawaida iliyodhibitiwa, Tanzania imefanya vizuri zaidi kuliko nchi nyingi zinazoibuka kwa haraka kiuchumi."

No comments:

Post a Comment