Moja ya vifaa vinavyotumika katika chumba cha Uzalishaji (Labor Ward) katika kituo cha Afya cha Maneromango vikiwa eneo la kusafishia kabla ya kutumika kwa shughuli za kitabibu. |
Hiki ndicho kitanda kinachotumika katika uzalishaji kwa wanawake wenye uhitaji na huduma ya Wajawazito wakati wa kujifungua.
Mmoja wa wahudumu wa Kituo cha Afya cha Maneromango akitimiza wajibu wake ilihali mazingira ya ufanyaji kazi katika kituo hich cha afya sio ya kuridhisha kwa wajawazito na watoto.
wahudumu wa kituo cha Afya Maneromango hutumia taa za kandili, chemli na mishumaa ili kuweza kupata mwanga nyakati za usiku pindi wanapohudumia wagonjwa kwakuwa kituo hicho hakina umeme tangu mwaka 2011.
Kwamujibu wa Afisa Afya wa Kituo hicho Bw. A. S. Sauni ni kwamba tangu betri mbili zilizokuwa zinatumika kwenye solar power ziharibike kumekuwa na hali mbaya kituoni hapo ya utoaji huduma kwa watoto na wajawazito hasa pindi wajawazito wanapokuwa wanajifungua.
Mmoja wa wanablog hii akiwa katika pozi baada ya kazi ngumu na safari ndefu toka Kisarawe mjini mpaka Maneromango!! |
Interview inandelea ambapo kamera yetu ilifanikiwa kuongea na muhudumu wa Afya Bi. Jane Denis.
|
No comments:
Post a Comment