|
Wiziri wa Elimu na Mafunzo Dr. Shukuru Kawambwa amesema wizara yake imeandaa matembezi ya hisani yenye lengo la kuchangisha fedha za ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike ili kuunga mkono kampeni ya ujenzi wa mabweni kwa wasichana inayoendeshwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). | |
Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari Dr. Kawambwa amesema uhaba wa mabweni katika shule za Sekondari unachangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kike nchini kwakuwa hukosa muda wa kujisomea kutokana na majukumu ya nyumbani.
|
Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu matembezi ya hisani yanayolenga kuchangisha fedha za ujenzi wa mabweni 30 ya wasichana katika shule za Sekondari nchini. |
hakuna kitu hapo kaka waziboreshe zilizokuwepo kwanza kabla ya kuchangisha kwa ajili ya nyingine... tanzania ina shule nyingi nawalimu wengi ila wizara inafanya uzembe na kupelekea nchi yetu kuwa ni nchi ya ajabu yenye kutoa wanafunzi waliomaliza darasa la saba (elimu ya msingi) lakini hawajui kusoma na kuandika... me nadhani hii wizara inahitaji marekebisho makubwa zaidi ya hayo ya kufanya harambee kwa ajili ya ujenzi...........
ReplyDelete