Wizara ya Nishati na Madini imesema uchimbaji wa madini ya Uranium utazingatia sera ya utunzaji wa mazingira ya mwaka 2000 na sera ya madini ya mwaka 2012 licha ya kuwa na upinzani mkubwa kutoka katika makundi ya wanaharakati ambao wanataka kusitishwa kwa uchimbaji wa madini hayo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Nishati ma Madini, Bw. Fadhil E. Kilewo, amesema wizara yake imeunda tume ya mionzi ya taifa (2003) ambayo itaratibu utolewaji wa elimu kwa jamii kuhusu namna ya kujikinga dhidi ya mionzi ya madini hayo.
No comments:
Post a Comment