Friday, November 30, 2012

MAKAMU WA RAIS WA MIGA KUFANYA ZIARA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI

Makamu wa Rais na Afisa Mkuu Uendeshaji wa shirika liitwalo Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA) la Benki ya Dunia, Bw. Michel Wormser, anatajia kufanya ziara ya kikazi ya siku tano katika nchini ya Tanzania na Afrika ya Kusini ifikapo mwezi December mwaka huu.

Taariafa kutoka Benki ya Dunia zinaeleza ziara hiyo ya Bw. Wormser, inalenga kuangalia namna uwekezaji dhamana unavyoweza kukuza sekta binafsi nchini katika nchi tajwa.

Inatazamiwa kuwa  Bw. Michel Wormser atakapofika nchini Tanzania atakutana na viongozi wa serikali na wale wa sekta binafsi ili kujadili fursa za uwekezaji katika kilimo cha biashara na nishati.

"Hivi karibuni taarifa ya Benki ya Dunia kukusu ukuaji wa uchumi wa Tanzania inaonesha haja ya kusaidia kilimo kiwe cha kibiashara ili asilimia 80 ya Watanzania wanaoishi katika maeneo ya vijijini waweze kufaidika na ukuaji wa uchumi," anasema Wormser.






No comments:

Post a Comment