Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka amekutana na wakazi wa tegeta katika ziara yake ya kikazi ambayo lengo lake ni kusikiliza na kutatua mgogoro wa ardhi uliopo kati ya wakazi hao na kiwanda cha kutengeneza Saruji (Twiga Cement).
Prof. Tibaijuka amewahakikishia wananchi wa kata Wazo na Bunju kuwa mgogoro huo wa ardhi utapatiwa ufumbuzi wa kudumu na kuwataka wananchi hao kutoa ushirikiano ili lengo la utatuzi wa mgogoro huo liweze kutimia.
No comments:
Post a Comment