Thursday, November 22, 2012

WATAALAMU WAJADILI KINGEREZA UDSM


EMBARGOED: No for newswire transmission, posting on websites, or any other media use
until November 20, 2012, 07:01pm EDT (November 21, 2012, 00:01 GMT)
Wataalamu mbalimbali kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na wadau wa elimu nchini wamekutana kujadili  ufundishwaji wa  somo la kingereza nchini.

Somo la kingereza nchini limekuwa gumzo  kutokana  na wanafunzi wa kada zote nchini kushindwa kufanya vizuri katika somo hilo jambo ambalo limekuwa likisababisha baadhi ya wanafunzi  kulichukia somo hilo.

Kwa mfumo wa utoaji elimu nchini darasa la kwanza mpaka la saba wanafunzi wamekuwa wakijifunza masomo yote kwa lugha ya Kiswahili ukitoa somo lenyewe husika la kiingereza. Na mara tu mwanafunzi huyo anapojiunga na kidato cha kwanza  mpaka cha nne basi hujikuta katika wakati mgumu kutokana na ukweli kwamba kila somo katika ngazi hii hufundishwa kwa lugha ya kiingereza, huku matokeo ya mitihani mbalimbali nchini yakiwa hayaridhishi.

No comments:

Post a Comment