Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda akifurahia na mke wake baada ya kutunukiwa shahada yake |
“Kama tutasubiri mashirika na taasisi za dini au watu binafsi wajenge vyuo vikuu vya mabweni, ni dhahiri wanafunzi wengi wasio na uwezo wa kulipia ada katika vyuo hivyo watasubiri kwa muda mrefu ili wadahiliwe au wakose kabisa nafasi kwenye Vyuo Vikuu,” alisema.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumamosi, Oktoba 27, 2012) wakati akiwahutubia washiriki wa mahafali ya 20 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) yaliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho eneo la Bungo, wilayani Kibaha, Pwani.
Alisema kuwepo kwa Chuo Kikuu Huria kumetoa fursa ya kuongeza udahili wa wanafunzi kwenye vyuo vikuu kwa kiwango kikubwa kwa vile kinaweza kuchukua wanafunzi wengi kwa wakati mmoja.
No comments:
Post a Comment